
Katika Uteuzi huo Dkt. Shein amewateua Bw. Haji Hamduni Omar kuwa
Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Luteni Kanali Mussa Mohamed Shaame
kuwa Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Bw. Abdi Omar
Maalim kuwa mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Shirika la Meli na
uwakala.
Aidha Dkt. Shein amewateua Bw. Hassan Abdalla Rashid kuwa Katibu
tawala wa wilaya ya micheweni na Bi. Miza Hassan Faki kuwa katibu tawala
wilaya ya mkoani .
Wengine ni Dkt. Juma Mohamed Salum kuwa Naibu Mkurugenzi Idara Habari
Maelezo katika Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Kanali
Ali Hassan Hamad kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo katika wizara ya Kilimo maliasili mifugo na Uvivu.
Uteuzi huo umeanza mara moja.
chanzo: zanzibar24.
Comments