
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Mafunzo ya Wanawake na Uongozi
kwa wanachama na viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini huko Amani Zanzibar, Dkt.
Mabodi alisema wananchi wa visiwa vya Zanzibar kwa sasa wanachohitaji
ni siasa za ushindani wa kisera katika kukuza kipato cha mwananchi
mmoja mmoja hadi taifa kwa ujumla.
Dkt. Mabodi alisema taifa lolote linalotamani kuendelea kiuchumi ni
lazima wananchi wake wakubali kwa vitendo dhana ya siasa za ustaarabu
katika kudumisha amani na utulivu wa nchi ili kufanya kazi za
kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo alisema ushindi wa CCM katika chaguzi
mbali mbali za dola unatokana na nguvu za Wanawake wa UWT katika kuunga
mkono harakati mbali mbali za kisiasa hadi kuhakikisha chama kinaingia
madarakani.
“ kila mtu ndani ya Chama Chetu anajua na kutambua mchango wa
Wanawake katika medali za kisiasa, wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kwa
kila kitu ikiwemo kujitokeza kwa wingi kupiga kura halali za kuiletea
ushindi CCM.
Pia nakuahidini kwamba nitaendelea kuwa nanyi bega kwa bega kwa lengo
la kuimarisha chama na jumuiza zake sambamba na kuwaletea wananchi
maendeleo ya kudumu.”, alisema Dkt. Mabodi.
Kupitia Mkutano huo Dkt. Mabodi aliwasihi viongozi na watendaji wa
Umoja wa Wanawake Tanzania kushuka ngazi za chini za uongozi hasa
matawi na mashina kwa lengo la kuratibu changamoto zinazowakabili
wananchi ili zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu na serikali.
Aliwapongeza viongozi wa UWT waliojitolea kuanzisha mafunzo ya
uongozi kwa wanawake wenzao ili wapate ujuzi wa kufanya siasa za
maendeleo zitakazowajengea ujasiri wa kujenga hoja imara zinazokubalika
katika ulimwengu wa siasa za ushindani.
Sambamba na hayo alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni
Rais wa Zanzibar Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kulinda
rasilimali za nchi hasa kuthibiti mianya ya usafirishaji wa Mchanga wa
Madini unaosababisha upotevu wa fedha nyingi za umma.
Akizungumzia Uchaguzi wa ngazi ya Wadi unaoendelea hivi sasa katika
Chama na Jumuiya aliagiza kwamba kamati zinazosimamia zoezi hilo zifanye
kazi ya ziada ya kuhakikisha wanapatikana viongozi safi wasiokuwa na
sifa za usaliti.
Mapema akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa
Mjini, Bi. Waridi Juma Othman aliahidi kuwa wanawake hao watatumia
vizuri mafunzo ya uongozi katika siasa kama muongozo wa kufanya kazi za
kisiasa kwa ufanisi mkubwa.
Akitoa neno la shukrani Mbunge wa Viti Maalum wanawake( MNEC),
Khadija Hassan Aboud alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo
wanawake wa CCM ili waweze kuzitumika vizuri fursa za uongozi
zinazopatikana ndani ya chama na serikali kwa ujumla.
Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum
wanawake( MNEC), Khadija Hassan Aboud kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Mjini, Faharia Shomari Khamis.
chanzo:zanzibar24.
Comments