Balozi Seif: SMZ haina nia ya kuwdhulumu wananchi wake.

baloziMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mtu yeyote ambae atasababisha migogoro ya Ardhi hata kama ni Kiongozi au Mwananchi wa kawaida.

Balozi Seif aliyasema hayo  chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa.


Akizungumzia kuhusu suala la mchanga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hatua iliyo chukuliwa na serikali ilikua na dhamaira yakuweka utaratibu mzuri wa matumizi bora ya rasilimli hiyo ambapo Jamii inapaswa kuelewa kuwa kadri inavyotumika kwa kasi rasilmali hiyo ndivyo inavyoendelea kumalizika.

Alisema Serikali haina nia ya kuwadhulumu Wananchi wake licha ya kuwepo malalamiko mengi ya Baadhi waliokuwa wakimiliki maeneo ya vitalu vya mchanga wakidai kuchukuliwa maeneo yao.

Hata hivyo Balozi Seif amewataka Wananchi wenye madai ya kuchukuliwa maeneo yao ya vitalu vya Mchanga wawasilishe vielelezo vyao katika Taasisi husika na aliwaahidi kero zao kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
chanzo: zanzibar24.

Comments