Askari sita wa Niger wauawa na magaidi katika mpaka wa nchi hiyo na Mali.


Viongozi wa Niger wametangaza kuwa askari sita wameuawa katika shambulizi la kigaidi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Mali.


Maafisa usalama nchini Niger wametangaza kuwa, shambulizi hilo limetokea katika mji wa Abala karibu kilometa 200 kaskazini mwa mji mkuu Niamey, karibu na mpaka na Mali. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, askari wanne wanatoka kikosi cha gadi ya ulinzi wa taifa na wawili ni polisi.


Mji wa Abala umekuwa ukishuhudia mashambulizi ya kigaidi. Kadhalika viongozi wa usalama nchini Niger wametangaza habari ya kuendelea mapigano baina ya wanachama wa kigaidi na askari wa serikali Alkhamisi ya jana katika eneo hilo na kwamba mapigano hayo yaliibuka baada ya askari kuanzisha operesheni zenye lengo la kuwasaka magaidi. 

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram limekuwa likiendsha harakati zake katika maeneo tofauti ya Niger, ikiwemo eneo la mpakani na nchi jirani ya Nigeria.

Licha ya nchi za eneo la Ziwa Chad kushirikiana katika operesheni kali za kuwasaka wanachama wa kundi hilo, lakini inaonekana kuwa genge hilo ambalo lilitangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) bado lina uwezo wa kutekeleza hujuma zake ndani na nje ya Nigeria.
chanzo:parstoday.

Comments