JESHI la Polisi linamshikilia kijana wa miaka 28 akituhumiwa kumbaka dada yake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali
JESHI la Polisi linamshikilia kijana wa miaka 28 aliedaiwa kumuingilia ndugu yake wa mama mmoja mwenye umri wa miaka 23 wakati akiwa anakoga chooni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alisema tukio hilo lilitokea Juni 26 mwaka huu saa 5.00 asubuhi Migombani mjini Unguja.


Alisema kijana huyo (jina limehifadhiwa) wakati mama yao akiwa ametoka yeye na ndugu zake wengine kuelekea sokoni, ndipo ndugu aliebakia nae nyumbani aliamua kwenda chooni kukoga na wakati akiwa anaendelea kukoga, mtuhumiwa aliingia chooni na kumkamata kwa nguvu na kasha kumuingilia.

Alisema baada ya mama yao kurejea, muathirika alimuhadthia mama yake ndipo walipoamua kwenda kituo cha polisi Madema kutoa taarifa na mtuhumiwa akatiwa nguvuni.

Kamanda Nassir, alisema kitendo kilichofanywa na kijana huyo ni cha kinyama na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya ushahidi kukamilika.

Aliwaomba wazazi na walezi kuwa na usimamizi mzuri katika familia zao hasa kwa watoto ili kuwaepusha na matatizo yasiyokuwa ya lazima.

“Jambo la msingi wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuepusha vitendo na madhara ya udhalilishaji wa kijinsia,” alisema.
Chanzo: Zanzibar Leo na zanzibariyetu.

Comments