Mbunge
wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe na Chama Chake
cha ACT Wazalendo wametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea kwa
ajali mbaya ya basi dogo ambalo limepelekea vifo vya wanafunzi 29,
walimu 2 na dereva mmoja wa gari hiyo.
"Moyo
wangu umesinyaa baada ya kusikia Taarifa za ajali ya watoto wetu huko
Karatu. Natoa salaam zangu za rambirambi kwa Wazazi wa wanafunzi wa
shule ya St. Lucky na Kwa ndugu na familia za walimu na wafanyakazi wa
shule waliopoteza maisha. Huu ni msiba mkubwa sana. Huzuni haielezeki.
Nawaombea Kwa Mola awape wazazi na ndugu wote moyo wa subira katika
mtihani huu. Ni msiba wa Taifa zima" alisema Zitto Kabwe
Katika taarifa ya Chama Cha ACT Wazalendo pia imetoa pole kwa wanafamilia, walimu
"Chama
cha ACT Wazalendo kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa ya
vifo vya wanafunzi, walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya awali na
msingi ya Lucky Vicent ya Jijini Arusha, vifo vilivyotokana na ajali ya
basi iliyotokea katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha. ACT Wazalendo
tunatoa pole kwa wazazi waliopoteza watoto wao, ndugu na jamaa
waliopoteza walimu na wafanyakazi wa shule hiyo, pamoja na watanzania
wote kwa ujumla. Pia tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapate
kupona kwa haraka" alisema Abdallah Khamis Afisa Habari wa ACT Wazalendo
chanzo:Mpekuziblog.
Comments