Zawa kutoa huduma Hospitali ya Chake Chake Pemba

Image result for MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR ZAWAMamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) tawi la Pemba imesem anaendelea kuboresha  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika hospitali ya Chake chake ili kuondoa kilio cha muda mrefu hospitalini hapo kutopata huduma hiyo kwa uhakika.

Hayo yamebainishwa leo na Afisa Mdhamini  Wizara ya ardhi mazingira maji na nishati Mh.Juma Bakari Alawi katika uzinduzi wa uchimbaji wa mtaro wenye lengo la kupeleka huduma hiyo katika hospitali ya Chake Chake .


Alawi amesema kuwa ZAWA kupitia wataalamu wake  katika kutafuta njia ya kupata maji ili kuihudumia hospitali hiyo wameamua kukiimarisha kisima kilichopo Madungu zstc ili kitoe huduma hiyo hospitalini hapo tu.

Aidha amesema jumla ya shilingi Milioni 40 na laki  nane za kitanzania  zitatumika kukamilisha mradi huo ambazo fedha hizo zimeombwa kutoka kwa mshirika wa maendeleo ambaye ni taasisi ya WATER FALLS ambayo makao makuu yake  yapo nchini Uingereza.

Amelezea kua uchimbaji wa mtaro, ulazaji wa  mabomba 7 ya nchi tatu, ununuzi wa 'Pump' na ujenzi wa Wellhead inategemewa sana katika kipindi cha wiki mbili kazi hizi itakua zimekamilika.

Hivyo amewaomba  mafundi na wataalamu wa ZAWA kuipa umuhimu kazi hiyo ili isichelewe zaidi ya  muda uliopangwa kukamilika.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Afisa uhusiano wa mamlaka hiyo Nd.Suleiman Anas Massoud amesema ZAWA imejizatiti kutokomeza ukosefu wa upatikanaji huduma ya maji safi na salama katika maenee yote  mijini na vijijini.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya ufundi wa mamlaka hiyo  Nd, Juma Ali Othman amesema kisima hicho kitatoa hudama massa 24 hospitalini  hapo pamoja na eneo la  madungu katika nyumba za Madaktari.

Amesema kuwa ni marufuku kwa watu wa kawaida kuunga  maji katika paipu hizo kwani  watakapounga watapunguza  nguvu ya utoaji wa huduma katika maeneo hayo.

Comments