Serikali ya Ujerumani imetiliana saini mkataba na Baraza la Manispaa ya Zanzibar wa ushirikiano wa kuendeleza miji kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari Mstahiki meya Khatib Abdulrahman Khatib na Mkurugenzi wa Manispaa Aboud Hassan Serenge wameseme mahusiano hayo yatasaidia kuimarisha na kusaidia mabadiliko ya tabia nchi ili kuendeleza mji wa Zanzibar kwa uwekaji taa katika maeneo mbalimbali,ujengwaji bustani za kisasa,ujengwaji vibaraza ambapo mradi huo wa ushirikiano wa kijamii katik kubuni na kupanga mipango ya maendeleo kwa kutoa huduma endelevu.
Hata hivyo Ujumbe ulipata fursa ya kuzungumza na wananchi marafiki wa Zanzibar na kubadilishana mawazo katika kutafuta miradi mbalimbali ya kijamii katika kuisaidia zanibar na kujitokeza wananchi wanaotaka kusaidia katika sekta ya elimu kufundisha shule za Zanzibar,kusaidia huduma za afya kwa kuanzisha kituo cha huduma za kensa,kuanzisha miradi ya mazingira na kuimarisha eneo la kikwajuni majumba ya mjerumani.
Katika safari hiyo Mstahiki Meya na ujumbe wake aliofatana nao walishiriki tukio la kihistoria ambalo ndio madhumuni ya ziara hiyo,kushiriki shughuli za michezo,kutembelea maeneo ya kihistoria na bustani ya mfalme Fredrick.
Zaidi ya Dolla Billion kumi 10 zitatumika katika makubaliano hayo ya kuendeleza mji wa Zanzibar katika mazingira yote.
chanzo: Zanzibar24
Comments