
Hayo yameelezwa na Naibu katibu mkuu wizara ya katiba sheria
utumishi wa umma na utawala bora Seif Shaaban Mwinyi kwenye hafla ya
makabidhiano ya jengo jipya ambalo lilifanyiwa ukarabati mkubwa na
kampuni ya ransi na kugharimu zaidi y a sh milioni 200.
Alisema kituo hicho kinatarajia kujengwa koani ambapo tayari serekali
ya mapinduzi Zanzibar imekwisha wapatia taasisi yao ya nyaraka kiwanja
na hatua ya sasa nikutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jingo hilo.
Alisema kwa hivi sasa tayari wamekwisha fanya mazungumzo na nchi
tafauti kama vile oman na irani ambapo wanasubiri wakati mipango ya
kutafuta nji nyengine inafanywa nahata michoro ya kituo hicho ipo
tayari.
Alisema kupatikana kwa jingo hilo kisiwani Pemba ni hatua muhimu
katika azma ya taasisi kuwa na kituo bora cha kutunzia kumbumbu kwani
kwa muda sasa Zanzibar inakabiliwa na tatizo la kituo cha kutunzia
kumbukumbu.
Mapema wakati wa kumkaribisha naibu katibu mkuu huyo Afisa mdhamini
wizara ya katiba sheria na utumishi wa umma Masoud Ali Mohamed alisema
kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu nimuhimu kwa sasa na baadae na hivyo
kuwataka watunza kumbukumbu kuzienzi ili ziweze kusaidia vizazi vinavyo
kuja.
Kwa upandewake engenia alie lifanyia ukarabati huo kutoka kampuni ya
ranscold Mohamed Shehe aliitaka wizara walio ikabidhi jingo hilo
kulikabua na kulifanyia ukarabati mara kwa mara ili liweze kudumu kwa
miaka mungi ijayo.
Alisema kwa muda wa miezi sita watakuwa chini ya uwangalizi wa
kampuni yake pale inapo tokea tatizo watarehebisha bure ilabaada ya hapo
itakuwa juu yawizara husika.
Comments