
Akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe Abdalla Maulid
Diwani Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na
Watoto Shadia Mohammed Suleiman
amesema katika utaratibu wa kawaida
muajiri anapaswa kutangaza nafasi za ajira kupitia vyombo vya habari
na iwapo hakupatikana mwananchi mwenye sifa zilizotajwa muajiri
anaruhusika kuajiri mfanyakazi wa kigeni na miongozni mwa sifa ni
kiwango cha elimu, ujuzi na uzoefu katika kazi husika.
Amesema wafanyakazi wa kigeni huajiriwa pale tu sifa kwa nafasi
zinazotakiwa kujazwa na wazanzibar wamekosekana sifa hizo kwa mujibu
wa sheria ya Ajira namba 11 ya mwaka 2005 kifungu 36 kifungu kidogo cha
A na B.
Hata hivyo Naibu Waziri Shadia ametoa wito kwa wazazi na walezi
kuwaandaa vyema vijana wao kielimu kujitahidi kuwasomesha watoto wao
fani mbalimbali ili kuweza kufikia viwango vinavyokubalika na kuingia
kwenye ushindani katika soko la ajira hasa katika soko la afrika ya
mashariki.
Hadi kufikia mwezi machi 2017 Jumla ya wafanyakazi 1026 wa kigeni
wameajiriwa zanzibar hasa katika sekta ya utalii na miradi maalum ya
ushirikiano baina ya serikali na washirika wa maendeleo katika nyanja
mbalimbali.
chanzo:Omar Zanzibar24
Comments