Wizi wa Mifugo washamiri Dimani.

Image result for Wizi wa Mifugo Uwepo wa wizi wa Mifugo uliokithiri katika shehia ya Dimani wilaya ya magharibi B ni miongoni mwa matatizo yanayo wasababisha wananchi wa shehia hiyo kushindwa kunufaika na mifugo yao.

Wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu wamekuwa hawanufaiki na mifugo yao kutokana na kuibuka kwa kundi la wizi wa mifugo nyakati za usiku.

Wakizungumza na Zanzibar24 Mwananchi Mwashamba Juma na Sheha wa Shehia hiyo Khatib Ame wamesema mbali na uwepo wa askari jamii lakini wanashindwa kuwadhibiti wezi kutokana na zana ndogo wanazotumia wakati wa kutekeleza wajibu wao.


”mwanzo kulikua na tatizo la wizi wa kuku, lakini baada ya kuwaekea mtego tulifanikiwa kumkamata mwizi mmoja lakini kwa sasa kumejitokeza wizi wa mifugo ikiwemo mbuzi, ukiamka asubuhi unakuta washaibiwa na washachinjwa na wanakuachia vichwa. Hakika hili jambo linatusikitisha sana” Wamesema wananchi hao.

Wametowa wito kwa Viongozi wa Shehia hiyo kuandaa utaratibu wa kuwapa mafunzo ya ulinzi askari jamii waliopo ili waweze kupambana na wezi hao wanaorejesha nyuma maendeleo ya wanakijiji.
chanzo:Zanzibar24.

Comments