Waziri wa Fedha: Zanzibar imepunguza kupokea misaada kutokana na kuimarika kwa vyanzo vya mapato vya ndani.

waziri wa fedha znz Khalid Salum Mohamed,Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Dk.Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar imepunguza kupokea misaada kutoka nje ya nchi kutokana na kuimarika kwa vyanzo vya mapato vya ndani ya nchi.

Akizungumza katika maadhimisho ya  wiki ya Mlipa kodi ilioandaliwa na ZRB amesema hatua hiyo imekuja baada ya wafanyakazi kuwa na mwamko wa kulipa kodi kwa hiari ambapo imesaidia ukuwaji wa Uchumi.


Amesema mwaka hadi mwaka serikali inaimarisha vyanzo vyake vya ndani na kupelekea kuweza kujitegemea  yenyewe bila ya kutegemea misaada ya wahisani.

Amesema matatizo yaliopo katika jamii ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi kwa wananfunzi yanatokana na baadhi ya Taasisi za Serikali na wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi kwa wakati.

Aidha ametoa wito kwa wafanyakazi wa taasisi zinzokusanya mapato ZRB na TRA kufanya kazi kwa uadilifu ili kuengeza ufanisi mzuri katika kazi zao pamoja na kuwacha tabia ya kutoa misamaha kwa wakwepa kodi pamoja na kuacha kutoa mizigo wakati wa usiku.

Jumla ya Bilioni mia nane zinatarajiwa kukusanywa kwa walipa kodi katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ambapo malengo yataweza kufikiwa.
chanzo:Zanzibar24.

Comments