
Wavuvi hao walipotea baada ya boti yao kukumbwa na upepo uliopelekea
kuzama, waliokotwa katika maeneno tofauti katika mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hasina Ramadhan Tawfiq
amewataja waliofariki kuwa ni Juma Omar Haji mwenye umri wa 42
aliyeokotwa pwani ya renco nungwi wilaya ya kaskazini A Unguja na Haji
Ngwali Sheha mwenye umri wa miaka 47aliyeokotwa katika pwani ya Mwambale
wilaya ya kaskazini A.
Aidha wavuvi wa nne kati ya sita walipatikana wakiwa hai na tayari wamepatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
chanzo: zanzibar24.
Comments