Wawakilishi washauri kuongezwa fedha kitengo kinachoshughulikia kesi za udhalilishaji.

baraza-la-wawakilishiWajumbe wa baraza la Wawakilishi wameeleza wasiwasi wao juu ya fedha  Million 55 zilizotengwa kuendeshea  kesi za  udhalilishaji kuwa ni kidogo na hazitoshi  kutokana kitengo hicho kuwa na mambo mengi ya kufatilia.

Wakizungumza  wakati wakichangia hoja za bajeti ya wizara ya kazi Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto katika kikao cha baraza la wawakilishi Wanu Hafidh Ameir, Asha Abdalla Mussa  na Hassan Khamis Hafidh wamesema, serikali iangalie kwa kina bajeti iliyotenga  kabla haijapitishwa  kuwa haitoshelezi kwani kesi za udhalilishaji zina kazi kubwa katika kufatilia na inahitajika Fedha za kutosha katika kukabiliana na vitendo hivyo.


Wamesema jamii sasa inakosa imani  na serikali kwani kila siku  vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vinashamiri bila ya kupatiwa ufumbuzi kwani kesi zinazofikishwa katika vyombo vya sheria hadi kupatiwa hukumu ni chache kuliko zinazobakia.

Aidha wamesema vitendo vya udhalilishaji vimekua vikiharibu taswira ya  Zanzibar hivyo serikali lazima itowe hukumu kali  kwa wanaotenda hayo ili kutoa fundisho  kwa watu hao.

Hata hivyo wamesema njia ya kumaliza matatizo hayo lazima serikali itenge pesa za kutosha kwa kitengo kinachofatilia kesi hizo na kuondoa dhana za utengemezi kutoka kwa wafadhili kwa jambo hilo.
chanzo:Zanzibar24

Comments