Wawakilishi waishangaa Serikali kuelekeza nguvu kwenye mradi wa camera badala ya miradi mengine ya maendeleo.

Wakichangia hutuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya
tawala za mikoa na Idara Maalumu,Wajumbe hao wamesema Fedha hizo
zinahitajika kuelekezwa katika shughuli nyengine za maendeleo ikiwemo
kuimarisha kwa miradi ya maji safi na salama pamoja na kununulia mashine
ya DNA itasadia kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi.
Wamesema kwa sasa kuna mambo muhimu katika jamii yanayohitaji
kupatiwa ufumbuzi hivyo ni vyema kwa serikali kutekeleza vipaumbele
vyake ikwemo kuimarisha mapambano dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia na
Watoto katika kuhakikisha mashine ya DNA inanunuliwa.
Aidha wametowa wito kwa serikali kuangalia kwa kina masuala ya
matumizi bora ya Fedha wakati wa kupanga bajeti za maendeleo ya ili
kupunguza malalamiko kwa wananchi.
Jumla ya Fedha Billioni 18 zimekusudiwa kutumika katika mradi wa
ufungaji wa Camera za Usalama ambapo kwa sasa mradi huo umeomba
kuengezewa Fedha zaidi.
Chanzo: Zanzibar24.
Comments