![Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto mbele) Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Daniel F.Kigeda(katikati mbele) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi (kulia mbele) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid,wakisimama pamoja na Wabunge wa Bunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,wimbo wa Taifa nchi za Jumuiya ukipigwa baada ya kumalizika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B"Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.](https://i0.wp.com/zanzibar24.co.tz/wp-content/uploads/2016/10/DSC_3674.jpg?resize=640%2C426)
Wakichangia hutuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya
tawala za mikoa na Idara Maalumu,wajumbe hao wamesema kuengezeka kwa
biashara ya magendo kunasababishwa na kikosi hicho kukosa vitendea kazi
vya kutosha ikiwemo usafiri wa boti za kufanyia doria.
Aidha wamesema mbali na wananchi kuwa na ushirikiano wa kuripoti
sehemu za ukanda wa bahari zinazotumika kuingwiza bidhaa hizo lakini
lengo la kukamatwa kwa wahalifu halifikiwi kutokana na vikosi hivyo
kusubiri zana za kutendea kazi kutoka katika maeneo mengine.
Aidha wametowa wito kwa viongozi wa KMKM kuwachukulia hatua za
kisheria watendaji wanaoshirikiana na waingizaji wa bidhaa za magendo
ili kuweza kunusuru kupotea kwa mapato yanayotokana na ukwepaji wa
ulipaji kodi wa bidhaa hizo.
Chanzo:Zanzibar24.
Comments