
Akiwasilisha hutuba ya Maoni ya Kamati hiyo kuhusu makadirio ya
Mapato na Matumizi ya wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na usafirishaji kwa
mwaka wa Fedha 2017/18 , Makamo mwenyekiti wa Kamati hiyo Suleiman
Sarhan Saidi amesema licha ya mafanikio makubwa juu ya kukamilika kwa
barabara mbalimbali lakini bado barabara hizo hazina viwango.
Aidha mbali na tatizo hilo idara ya ujenzi na Utunzaji wa Barabara
imekabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kutendea
kazi , uchakavu wa mitambo ya kutengenezea lami jambo linalopelekea
barabara zinazojengwa kuhatarisha maisha ya wananchi hususan katika
kipindi cha mvua.
Hata hivyo amesema ili kuondowa matatizo hayo ni vyema kwa serikali
kutenga bajeti ya utunzaji na Matengenezo ya Barabara ili kuweza
kuzifanyia matengenezo barabara ambazo zipo katika hali mbaya licha nya
kuwa hazijapangwa kutengenezwa katika mwaka wa fedha 2017/2018.
chanzo:Zanzibar24
Comments