Wavuvi 7 wanusurika kufa baada ya ngalawa yao kuzama.

Watu saba ambao ni wavuvi wamenusuruka kufa baada ya ngalawa yao kuzama maeneo ya kisiwa cha chumbe walipokuwa wakiendelea na shughuli zao za uvuvi.

Kamanda Moh’d Ali wa KMKM amesema wakati walipokuwa wanaendelea na doria zao za kawaida ndipo walikishuhudia chombo ambacho kimepakia wavuvi hao kinazama na ndipo walipoenda kuwaokoa na kufanikiwa kuwapata wote wakiwa salama.


Nae nahodha wa chombo hicho Antony Mkaringa Mtama alisema chanzo cha ajali hiyo ni upepeo mkali ambao uliyombisha chombo hicho kuyumba na kukisababishia kuzama.

Wavuvi walionusurika kufa ni pamoja na Said Abdallah Fadhili Mo’d Haji,  Fokas Mtata, Mtumweni na wawili ni abiria ambao bado hawajatambulika majina yao.
chanzo: zanzibar24.

Comments