
Akizungumza katika Kongamano la 9 ambapo kwa Zanzibar ni la kwanza
kufanyika lililofanyika katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la
zamani la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani amesema katika
kuelekea katika ibada ya funga waislamu hawana budi kujiandaa kwa
mambo mema na kuzidisha unyenyekevu kwa Allah (S.W)
kwani ndio nguzo muhimu pamoja na kusoma kitabu kitukufu Qur-ani.
Hata hivyo amesema waislamu wanajukumu kubwa kwa mwenyezi mungu
katika kutekeleza ibada, hivyo umoja na mshikamano ndio ngao kubwa
itakayo waunganisha na wasikubali nchi yao ikawa na matabaka yatakayo
sababisha mtafaruku na kupelekea nchi ikawa katika machafuko.
Kwa upande wake Mufti mkuu wa Zanzibar Saleh Omar Kabi amewasisitiza
waumini wa kiislamu kuwa na imani katika mwezi wa ramadhani kwa kuwacha
matendo machafu yatakayo batilisha funga zao badala yake kushiriki
katika mambo mema ikiwemo kusoma qur-ani,kutoa sadaka pamoja na kuwa
waja wema katika maisha yao yote.
Akitoa salam za serikali kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein Waziri wa Nch Ofisi ya Rais
Katiba,Sheria,Utumishi wa umma na utawala bora Haroun Ali Suleiman
amesema Serikali itakuwa bega kwa bega kwa wataoshiriki katika kuchafua
mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ili
kutoa fundisho wa kuheshimiwa mwezi huo.
Pia Haroun amesema kutokana na umuhimu wa kongamano hilo la
kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani serikali itahakikisha kila mwaka
kongamano kama hilo linafanyika ili kuwajenga wananchi wa kiislamu.
Kongamano hilo la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani
limeandaliwa na Ofisi ya Mufti wa Zanzibar liliwakutanisha waislamu
mbalimbali Zanzibar.



chanzo:Zanzibar24
Comments