
Aidha, katika kukoleza kasi ya msako huo, jeshi hilo limetangaza
kutoa dau nono la Sh milioni 5 kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa
watuhumiwa hao. Hayo yalibainika jana mjini hapa kupitia taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Abdulshakur Makeo
aliyetajwa kuwa ni mwanzishi wa harakati za mauaji Ikwiriri, wilayani
Rufiji. Wengine ni Faraj Nangalava, Anaf Kapera pia anafahamika zaidi
kama Kapelo, Said Ngunde, Omar Matimbwa, Shaaban Kinyangulia, Haji
Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Uponda, Rashid Mtulula, Shehe Hassan
Mzuzuri na Hassan Njame
Zaidi ya watu 31 wamepoteza maisha, wakiwemo viongozi na makada wa
chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na mauaji yanayoendelea
Mkoani Pwani.
chanzo:zanzibar24.
Comments