
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.
Ikiwa
itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi
kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50
walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.
Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa
Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake,
wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.
Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.
Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao
hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa
kujitoa mhanga.
Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa
wanaume, ndio ukumbua mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua
watu 18,000
Ukumbi huo hutumiwa kuandaa tamasha za manyota wakuu kama Ariana
Grande nyota wa runinga mwenye umri wa miaka 23 ambaye sasa ni nyota wa
muziki wa pop.
chanzo:Bbc.


Comments