
Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya wateja hao wamesema tokea kufungwa kwa banki hiyo hakuna taarifa yoyote waliyopewa kuhusu kupatikana kwa fedha zao.
Kwa upande wake Mshauri Bodi ya Bima ya Amana Rashid Mrutu ambayo imepewa dhamana ya kuwa mfilisi wa Benki hiyo amewataka wadai na wadaiwa kuwa wavumilivu wakati Mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao.
Uamuzi huo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya kuifutia lessen Benki hiyo ya FBME umetolewa baada ya hukumu ya kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa ikiikabili benki hiyo kutolewa.
Itakumbukwa mwaka 2014, Mtandao wa Kudhibiti Uhalifu wa Masuala ya Fedha (FinCEN) wa Marekani uliitaja FBME kuwa taasisi inayojihusisha na utakatishaji fedha hivyo kuizuia kutoa huduma nchini humo.
chanzo:zanzibar24.
Comments