
Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru,
kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko
Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.
Wasichana hao
ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka
shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa
Nigeria.
Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la
Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya
ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na
mpaka na Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC
Stephanie Hegarty kutoka Lagos.

Ni sehemu ya maelfu ya watu ambao wametekwa nyara na wanamgambo hao, walioanzisha vuguvugu hilo miaka minane iliyopita.
Utekaji nyara huo ambao ulifahamika baadaye kama "Chibok girls"
ulisababisha kilio kikubwa kote duniani na kampeini za kutaka waachiwe
huru ikatanda kote katika mitandao ya kijamii.
Kabla ya hatua hii ya hivi punde ya kuwaachia wasichana hao, inakisiwa kuwa zaidi ya wasichana 195 wangali hawajulikani waliko.
chanzo:Bbc.
Comments