Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo amewataka viongozi wa chama hicho wilaya kuwatimua wasaliti wote waliokosaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015 ili uchaguzi ulioanza ngazi ya mashina ufanyike kwa amani.
Akizungumza na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, kata, matawi na mashina akiwa kwenye ziara ya kuangalia maendeleo ya uchaguzi ngazi ya mashina na maandalizi ya uchaguzi ngazi ya matawi wilayani Mpwapwa na Kongwa mkoani Bulembo amesema wasaliti hao walikiumiza chama wakati wa uchaguzi na makovu hayajapona.
"Huwezi kuwabeba watu ambao walitusaliti na kututia madoa, tumewaondoa ngazi ya Taifa na ninyi watimueni haraka sana hawatufai,"amesema Bulembo.
Amesema huenda vikao vilivyofanyika ngazi ya mkoa havikuwabaini na kuwachukulia hatua lakini viongozi ngazi za wilaya na kata wanawajua hivyo ni vyema wakawekwa pembeni ili wanachama wachukue fomu wakiwa huru.
chanzo:Mwanachi.
Comments