Wananchi wa Shehia ya nyamanzi waiyomba Serikali kuimarisha ulinzi katika maeneo yao.

HABARIWananchi wa Shehia ya nyamanzi Wilaya ya Magharib B Unguja wameiomba Serikali kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ya ukanda wa Bahari ili kuzuia Bidha za magendo zinazoingizwa kwa wingi katika maeneo yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ziara ya kutembelea Kijiji cha Nyamanzi na Dimani Sheha wa Shehia ya Nyamanzi Seif Muhammed Hassan amesema mbali na uwepo wa ulinzi shirikishi katika maeneo yao lakini wanashindwa kukabiliana na hali hiyo kutokana na kukosa vifaa vya kitaalamu vya kulindia maeneo hayo.


Hata hivyo amesema mara kwa mara wamekuwa wakishuhudia Bidhaa mbali mbali za magendo zinaletwa ikiwemo Mbao za kujengea pamoja na  Madawa ya kulevya ambayo ni hatari kwa vijana wao.

Aidha amesema pindipo Serikali itaimarisha ulinzi katika maeneo ya ukanda wa bahari itasaidia kuwakamata kirahisi watu wanaoingizwa bidhaa kinyume na sheria zilizowekwa.

Ziara hiyo ya siku moja iliandaliwa na  Clab ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC kwa wandishi wa habari kutembelea Shehia za Dimani na Nyamanzi kwa lengo la kujua umuhimu wa kuandika habari za Vijiji ikiwa ni sehemu ya Shamrashamra ya kuadhimisha Siku ya uhuru wa Vyombo vya habari nchini.
Nchanzo: Zanzibar24.

Comments