Hayo yameelezwa na msemaji wa jeshi la
Chad ambaye amebainisha kwamba, kambi ya jeshi iliyoshambuliwa na
wanamgambo wa Boko Haram ipo katika eneo linalopakana na Nigeria.
Kanali Azem Bermandoua ameeleza kuwa,
mbali na wanajeshi wao wanane kuuawa katika shambulio hilo, kuna wengine
28 waliojeruhiwa pia katika hujuma hiyo ya kijeshi ya Boko Haram.
Jeshi la Chad limeeleza kuwa,
limeimarisha usalama katika maeneo hayo baada ya shambulio hilo la
wanamgambo wa Boko Haram wenye makao yao nchini Nigeria.
Shambulio hilo la Boko Haram linafanyika masaa kadhaa tu baada ya
António Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kulitaka kundi la
kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria kuhitimisha ukiukaji wake wa
haki za watoto.
Kundi la Boko Haram lilianzisha
mashambulizi dhidi ya maeneo ya umma na taasisi za serikali huko
kaskazkini mwa Nigeria mwaka 2009 na baadaye mwaka 2015 likapanua
mashambulizi hayo hadi katika nchi za Chad, Cameroon na Niger.
Zaidi ya watu elfu 20 wameuwa hadi sasa katika mashambulizi hayo na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi.
chanzo:parstoday.
Comments