Wakulima wa mwani Pemba wakabithiwa vitendea kazi.

Image result for wakulima  wa mwani pemba.
Wakulima wa mwani mkoa wa kaskazini pemba wamekabidhiwa boti kumi[10] ambazo zitasaidakuendeleza shughuli zao za  kilimo chao.


Akikabidhi boti hizo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba OMAR KHAMIS OTHMAN amesema lengo la kukabidhi boti hizo ni kuendeleza Kilimo cha Mwani na kujiongezea kipato katika familia zao.



Aidha amewataka wakulima hao kujipanga na kuhakikisha Boti hizo wanazifanyia ukarabati kwa kutumia nguvu zao  ili ziweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu huku akiwasisitiza kutoziuza.



Wakizungumza na mara baada ya kukabidhiwa boti hizo
kwa Niaba ya wakulima wenzao   SHAIBU KASSIM HAMAD  na KHADIJA WILSON MAIGE wamesema Boti hizo zitawawezesha kuongeza uzalishaji wa zao la mwani.



Sambamba na hayo,wakulima hao wamesema kwamba zao la Mwani limewatia hasara kubwa kutokana na msimu huu wa mvua kwani baada ya kuuwanika huchelewa kukauka na hatimae huoza majumbani mwao kutokana na kukosa jua la kutosha.


Mara kwa Mara wakulima wa mwani Kisiwani Pemba hukabidhiwa vifaa mbali mbali kwa ajili ya kupambana na Kilimo hicho ili kuweza kupata mavuno bora kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

Comments