Waziri wa Mambo yanje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Augustine Mahiga amewataka
wajasirimali Kisiwani Pemba kuzutumia vyema fursa zilizopo ili kuweza kumudu
ushindani katika soko la Afrika Mashari.
Waziri Mahiga ameyasema hayo wakati akifungua
semina ya siku nne kuhusu utoaji wa
elimu kwa wajasiriamali na wafanya biashar
juu ya mtangamano wa Jumuiya Afrika Mashariki ambayo imefanyika katika
ukumbi wa kiwanja cha Gombani Kisiwani Pemba.
Amesema kuwa wajasirimali na wafanyabiashara
wanafursa kubwa zitakazo wasaidia kuingia katika soko la pamoja kutokana na
kuwa nchi ya Tanzania ndio inayo ongoza kwa utoaji wa bidhaa bora
zenyekuzingatia vigezo vinavyo hitajika.
Amefahamisha kuwa kuundwa kwa Soko
la Jumuiya ya Afrika Mashariki nikuwawezesha wajasiriamali na wafanya
bishara hao kuweza kuongeza ushindani kwa nchi zinazo unda shirkisho hilo.
Nae naibu Warizi wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Zanzibar Mh Khamis Juma Maalim amesema kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa tangu
kuanzishwa kwa soko la pamoja kwani limeweza kuwasaidia wajasiriamali kuweza
kushiriki katika maonyesho mbali mbali hususan yale yanayo wahusu
wajasiriamali.
Aidha ameeleza kuwa nimuda muwafaka kwa wajasirimali na wafanya biashara
Kisiwani Pemba kuyatumia vyema mafunzo yao ili yaweze kuwaletea mabadiliko
katika shughuli zao.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Soko la Jumapili Chake Chake Pemba Khamis
Suleiman Masoud kwaniaba ya wafanya
biashara na wajasiriamali wenzake wameishukuru Serekali ya Mapinduzi Zanzibar
na ile ya Muungano kwa kuwapatia mafunzo yatakayo wawezesha kubuni miradi
itakayo wasaidia kuitangaza vyema tanzania na kuahidi kuyatumia ipasavyo
mafunzo hayo.

Comments