Waokoaji
wanasema boti kadhaa zilikumbwa na dhoruba na kuzama ghafla zikiwa na
abiria karibu 200.
Kamanda wa Gadi ya Pwani ya Italia, Cosima Nicastro
amesema, wameopoa miili 20 majini huku kundi la uokoaji la MOAS likisema
limepata miili 34 aghlabu yao wakiwa ni watoto wadogo.
Waokoaji
wanasema, karibu boti 15 zilizokumbwa na dhoruba zilikuwa na abiria
karibu 1,700.
Mwaka
huu karibu watu 1,300 wamepoteza maisha mwaka huu wakivuka moja ya
maeneo hatari zaidi baharini kwa lengo la kukimbia umasikini na vita
barani Afrika na Mashariki ya Kati.
Habari zinasema kuwa, mwaka jana zaidi ya wahajiri 5,000 hususan wa
Kiafrika walipoteza maisha kwa kuzama baharini katika bahari ya
Mediterania wakiwa katika safari hizo hatari za kuelekea Ulaya
wanakodhani kwamba watapata maisha mazuri na ajira.
chanzo:parstoday.
Comments