Kitendo hicho kimefanya fikra za walio wengi kutoa radiamali wakisema
kuwa, Marekani inakusudia kukwamisha juhudi za mapambano hayo dhidi ya
ugaidi.
Inaelezwa kuwa katika mwenendo wa mafanikio ya jeshi la Iraq dhidi ya magaidi, harakati ya Hashdu sh-Sha'abi imefanikiwa kukomboa mji wa al-Qairawan, magharibi mwa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh.
Inaelezwa kuwa katika mwenendo wa mafanikio ya jeshi la Iraq dhidi ya magaidi, harakati ya Hashdu sh-Sha'abi imefanikiwa kukomboa mji wa al-Qairawan, magharibi mwa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh.
Katika siku kadhaa zilizopita
harakati hiyo ya wananchi ilianzisha operesheni za kuukomboa mji huo wa
kistratijia ulio umbali wa kilomita 90 magharibi mwa Mosul katika mpaka
wa Iraq na Syria, huku operesheni hizo zikizaa matunda Jumannde
iliyopita.
Baada ya miezi kadhaa ya vita na mapigano makali, jeshi la Iraq
limezidi kusonga mbele huko magharibi mwa mji huo ambao ni makao makuu
ya mkoa wa Nainawa (Nineveh) kaskazini mwa Iraq kwa ajili ya kuukomboa
kikamilifu mji huo.
Katika uwanja huo ndege za kivita za Marekani zimewalenga
wanamapambano wa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi waliopo
katika maeneo ya mpakani ya nchi hiyo na Syria.
Njama hizo za Marekani
zinatekelezwa katika fremu ya siasa za chuki za Washington katika eneo
kupitia misaada yake kwa nchi zinazopambana na ugaidi (yaani Iraq na
Syria.) Marekani inatoa nara za kupambana na ugaidi katika hali ambayo
kuna nyaraka mbalimbali zinazothibitisha kwamba makundi mengi ya kigaidi
likiwemo genge hatari la Daesh (ISIS), yameanzishwa na kulelewa na
idara za ujasusi za Marekani.
Katika kitabu chake cha 'Machaguo Magumu'
Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani alikiri
wazi kwa kusema: 'Ni sisi tuliounda kundi la ISIS.' Mwisho wa kunukuu.
Hata hivyo suala la kuzingatia ni hili kwamba, tangu kulipoundwa
muungano huo bandia, utendajikazi wake umebainisha kuwa, malengo yake
makuu sio kumaliza makundi ya kigaidi hususan Daesh (ISIS), kama
inavyodaiwa na Washington, bali ni kuyaimarisha na kuyapa nguvu zaidi
makundi hayo.
Kwa msingi huo katika hatua ya mwisho ya mapambano dhidi
ya ugaidi nchini Iraq, Marekani inafanya ukwamishaji mambo kwa kuwa
serikali ya Trump imekusudia kuzuia operesheni za kulimaliza kabisa
kundi la Daesh bali inafanya juhudi za kuliimarisha zaidi kundi hilo la
ukufurishaji nchini Iraq.
Mbali na hayo ni kwamba hatua ya Marekani
kushambulia maeneo ya askari wa harakati ya Hashdu sh-Sha'ab mjini Mosul
inaibua maswali juu ya sababu kuu ya uadui wa Marekani kwa harakati
hiyo.
Harakati ya Hashdu sh-Sha'ab imelengwa na hujuma za kila upande za
Marekani katika hali ambayo jeshi la Iraq limefikia mafanikio makubwa
ya kukomboa maeneo mengi ya nchi hiyo yaliyokuwa chini ya udhibiti wa
kundi la ukufurishaji na kigaidi la Daesh kupitia ushirikiano wa bega
kwa bega na harakati hiyo.
Itafahamika kuwa, mji wa Mosul ambao ulikuwa mji wa mwisho kwa wanachama
wa kundi la Daesh kuonyesha nguvu zao, umekuwa pia wa mwisho kwa
harakati ya Hashdu sh-Sha'ab kuonyesha nafasi yake muhimu katika
mapambano yake dhidi ya magaidi hao. Kabla ya hapo Hashdu sh-Sha'ab
ilikuwa na nafasi chanya katika ukombozi wa mikoa ya al-Anbar, Diyalah
na Salahd-Din kutoka mikononi mwa genge hilo.
chanzo: parstoday.
Comments