Zeid Ra'ad al-Hussein, Kamishna wa Haki za Binadamu wa UN amesema
kiungo huyo wa kati raia wa Ghana ni mfano wa kuigwa ambaye ametoa ari,
motisha na wakati huohuo changamoto kwa watu wengi haswa kwa afisi hiyo
ya Umoja wa Mataifa, kutokana na kitendo chake hicho.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Ganeva nchini Uswisi, afisa
huyo wa Umoja wa Mataifa amelitaka Shirikisho la Soka Duniani FIFA
kuliangalia kwa makini suala la wachezaji kubaguliwa na kudhalilishwa
kwa misingi ya rangi zao wakiwa uwanjani.
Muntari, aliondoka uwanjani baada ya refa kumpa kadi ya manjano,
alipolalamika kuwa baadhi ya mashabiki wakiwemo watoto walimrushia
cheche za maneno ya kibaguzi, wakati wa mechi ya Ligi ya Serie A kati ya
timu yake na klabu ya Cagliari.
Huku akionekana kukerwa na kitendo
hicho cha ubaguzi, Sulley Muntari aliwakabili mashabiki wa klabu ya
Cagliari na kufoka kwa sauti akisema "Hii ni rangu yangu!" huku akiashiria rangi ya mkono wake..
Kiungo huyo wa zamani wa Ghana mwenye umri wa miaka 32, alimuomba
refa Daniele Minelli asimamishe mechi hiyo ya Jumapili kutokana na
kitendo hicho cha kibaguzi, ili kuonyesha mfano mwema kwa mashabiki.
Hata hivyo refa huyo badala yake alimpa kadi ya manjano katika dakika ya
89, hatua iliyosababisha mchezaji huyo wa zamani ya timu Portsmouth na
Sunderland kupinga kwa kuondoka uwanjani.
chanzo:parstoday.
Comments