
Mwanamke mmoja jijini Dar es salaam aliejitambulisha kwa jina
la Sarafina anafanya kazi ya kuosha watu miguu nje ya soko la Mabibo
mara tu wanapotoka kununua bidhaa mbalimbali katika soko hilo.
Mwanamke huyo anasema kuwa uchafu wa sokoni hapo ndio ulimpa wazo la
kuanzisha biashara hiyo ambayo inamuendeleza kimaisha kwa kipindi hichi
cha mvua.
Anasema kuwa mtu mmoja humnawisha kwa shilingi 100 na kwa siku
huingiza kiasi cha shilingi elfu 30 na kufanikiwa kuajiri vijana wanne
ambao wanamsaidia kufanya kazi hiyo sokoni hapo.

chanzo:zanzibar24.
Comments