
Taarifa kutoka ikulu ya marekani zinasema kuwa Donald Trump na
Vladimir Putin wamekubaliana kuwa vita vinavyoendelea Syria vimefikia
katika hatua mbaya na pande zinazohasimiana hazina budi kukaa pamoja na
kumaliza mapigano hayo.
Viongozi hao wawili pia wamejadili namna
ya kufanya kazi kwa pamoja kuliangamiza kundi la IS pamoja na suala la
nyuklia la Korea ya Kaskazini.
Haya ni maongezi ya kwanza kwa viongozi hao wawili, tokea Trump alipoishambulia Syria inayoingwa mkono na Urusi.
chanzo:Bbc.
Comments