Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo
haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa
kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo
ameyasema jana Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa
waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na
TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye
ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko
kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi anayopaswa
kulipa Diamond, na kwa bahati nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye
mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu
kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu
umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya
kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa
hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi
ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo
mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na
mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu
wasiogope. Alisema.
Awali
akifungua semina hiyo, Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga
uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA,
katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali
kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
“Najua
kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi
watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu
walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia
taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.
Bwana
Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye
mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi,
makampuni na taasisi za umma.
“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema
na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya
kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka
kwa watalamu wa kodi wa TRA.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments