SMZ yakabidhiwa tani mia moja ya tende kwa ajili ya Ramadhani.

Mfalme Salman Bin Abdul-azizi ametoa msaada wa tende tani mia 100 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ikiwa ni sadaka kwaajili  ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akikabidhi msaada huo Naibu Balozi kutoka Saudi Arabia Bandar Al-hadhani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais katiba,sheria,utumishi wa umma na utawala bora amesema kila ifikapo mwezi kama huu Saudi arabia hutoa msaada katika sehemu mbalimbali ikiwemo Zanzibar ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi hasa wanyonge.

Kwaupande wake Waziri Haroun Ali Suleiman ameushukuru Ufalme Salaman kwa msaada huo ambao utasaidia  waislamu wengi katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Amesema Salman amekuwa mdau mkubwa kwa serikali yake kwa  kuisaidia Zanzibar katika kipindi cha ramadhani  nahata baada ya  hijja hutoa msaada wa nyama.
chanzo: Zanzibar24

Comments