Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Imeahidi kuyafanyia matengenezo Madaraja yote yalichakaa na yalioharibiwa na mvua pamoja na Barabara zinazotuama maji ili kuwanusuru wananchi na Majanga yanayoweza kujitokeza ikiwemo kusababisha ajali kwa vyombo vya moto.
Akizungumza na waandishi wa habari Baada ya ziara ya kutembelea madaraja Matatu yaliopo katika Barabara ya Kitope Mkoa wa Kaskazini “B” Unguja, katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe amesema madara hayo tayari yameshakuwa ya zamani na mengi kuathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Aidha amesema Barabara hiyo pamoja na Barabara ya Fuoni kwenda Tunguu pia ziko katika mpango wa kutengenezwa baada ya matengenezo ya dharura yatakayofanya ili kuwarahisishia wananchi Huduma za usafiri.

Aidha ametowa wito kwa madereva na wananchi wanaotembea kwa miguu katika Barbara hizo kuwa waangalifu wakati wa safari zao ili kujiepusha na ajali zinazoweza kujitokeza.
Wakati huo huo katibu mkuu huyo ameagiza watendaji waliopo chini yake kuengeza majengo ya vyoo katika jengo la leseni Mwanakwerekwe ili kupunguza usumbufu uliopo kwa wananchi na wafanyakazi waliopo katika ofisi hiyo.

Miongoni mwa maeneo yalitembelewa katika ziara hiyo ya siku moja,ni pamoja na mto wa kibonde mzungu na Madaraja yaliopo katika Barabara ya kitope.
chanzo: Zanzibar24.
Comments