Skuli ya msingi Bububu hatarini kutoweka.

HABARISkuli ya msingi Bububu ipo hatarini kupotea kutokana athri kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi hali ambayo imewatia hofu baadhi ya viongozi wa misitu na kuamua kurudisha haiba nzuri ya eneo hilo.

Akizungumza na Zanzibar24 mwalimu wa skuli hiyo Ame Haji Vuai na kusema eneo la skuli ya msingi Bububu limekua na athairi kubwa dhidi ya uchafuzi wa mazingira na kuamua kupanda mikoko ili kulinusuru eneo hilo kuharibika kabisa.


Nae Omar Khatib kutoka idara ya misitu na mali amesema kuwabinaadam ni nchanzo kikuu cha uharibifu wa mazingiza pamoja na kuwa elimisha wanafunzi wa skuli hiyo juu utunzaji wa mazingira yanayowazunguka na kupanda miti.

“Upandaji huo wa mikoko ni muhimu kama ulivyo upandaji wa miti mengine kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa mazingira.

Zaidi ya miti alfu kumi aina ya mikoko imepandwa katika eneo la skuli na fukwe kwa lengo la kutudisha mazingiora na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
chanzo: zanzibar24.

Comments