
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Suleiman Hassan
Suleiman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa Tukio hilo
limetokea jana majira ya saa tisa na dakika arobaini jioni huko
Bumbwini bondeni Wilaya ya kaskazini B.
Kaimu Kamanda amemtaja Marehemu kuwa ni Taifa Mohamed Ali mkazi wa Bumbwini bondeni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kabla ya kifo chake Marehemu alikua nyumbani kwake ambapo baada ya
kumaliza kupika na kuanza kula inasadikiwa alikwenda kuufunga mlango wa
geti huku waya wa umeme ulioko chini ya geti hilo ukiwa umechunika ngozi
ndipo alipopigwa shoti na kunasa na kusababisha kifo chake.
Mtoto aliyenusurika kufa ametambulika kwa jina la Ali Mohammed Ali
mwenye umri wa miaka 3 mkazi wa Bumbwini. Tayari mwili wa marehemu
umefanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Mnazi mmoja na kukabidhiwa
ndugu zake kwa mazishi.
chanzo: zanzibar24.
Comments