Serikali yatoa onyo kali kwa walimu wa Madrasa watakaojihusisha na vitendo vya Udhalilishaji.

madrasa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imesema haitafumbia macho vitendo vya udhalilishaji ambavyo vinahusishwa na baadhi ya  walimu wa madrasa  na badala yake itawachukulia hatua za kisheria watakao husika na vitendo hivyo.

Akizungumza katika Semina kwa walimu wa Madrasa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais katiba,sheria,utumishi wa umma na utawala bora Khamis Juma Mwalimu amesema kumezuka tatizo la walimu wa madrasa kujihusisha na vitendo  vya udhalilishaji kwa kuwalawiti na kuwadhalilisha watoto jambo ambalo linawatia doa na kubadilisha haiba ya walimu wengine.

Amesema ipo haja kwa walimu wa madrasa kurudi katika maadili yao ya uwalimu kwani dhamana walio ichukua ya kujitolea kuwasomesha watoto ni kubwa kwa mwenyezi mungu na itawapandisha katika daraja kubwa hivyo waache kabisa tabia hiyo ili kuzirejesha imani za wazazi.
Kwa upande wao baadhi ya walimu walioshiriki semina hiyo wametoa wito kwa walimu wote nchini wenye tabia hizo za kinyama kuwacha mara moja kwani inatia doa tasnia ya Uwalimu hasa wa madrasa kwa kuonekana hawana thamani katika jamii kwa kazi yao kutokana na baadhi yao kujihusisha na vitendo vya  kuwadhalilisha watoto katika vyuo.
chanzo: Zanzibar24

Comments