Serikali imesema itapelekea fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/17 kadri inavyozipata kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji amesema hayo leo (Jumanne) bungeni kwamba Serikali itaendelea kutoa fedha za miradi kwa kadri wanavyopata.
Dk Kijaji alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje alitaka kufahamu ni lini fedha za miradi zitapelekwa katika mikoa na wilaya ili miradi iliyoanza kutekelezwa imaliziwe.
Pia katika swali lake la msingi aliomba kufahamu ni sababu gani zinazofanya Serikali kuchelewesha kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika mikoa na wilaya.
chanzo:Mwananchi.
Comments