SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha Uvuvi wa Pweza Pemba.

Image result for pwezaSERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Sekta ya Uvuvi imedhamiria kueka mpango maalum wa kusimamia na kuimarisha Uvuvi wa Pweza, ili kusaidia kunyanyua hali za wananchi kiuchumi pamoja na kuongeza pato la taifa.

Hayo yameelezwa na Afisa mkuu Idara ya maendeleo Uvuvi Pemba, Sharif  Mohammed Faki, katika mkutano wa wafanyabiashara ya wavuvi wa Pweza, huko Weni Mkoa wa Kskazini Pemba.


Amesema kupitia mradi wa Swiofish unaoshughulika na masuala ya uhifadhi wa samaki, kupitia kamati za wanavijiji  kwa kufuta utaratibu maalum wa viwango vya Pweza vilivyowekwa kulingana na sheria za Uvuvi na sheria za maeneo ya hifadhi.

Sambamba na hayo, amesema kuwa, Serikali itaanzisha vituo vya barafu ili kuhifadhi na kuanzisha viwanda vya kusarifu Pweza,kuwawezesha wafanyabiashara waweze kuuza katika masoko ya ndani na nje, jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kunyanyua biashara ya pweza nchini.

Akichangia katika mkutano huo, Mohammed Suleiman Ntale, ambae ni mfanyabiashara ya Pweza katika Kampuni ya TANPESCA, ameiomba Serikali pia kuangalia uwezekano wa kuwasaidia vifaa vitakavyowawezesha wavuvi kwenda baharini na kupata Pweza wakubwa wenye viwango vinavyokubalika.

Nae Afisa usarifu wa mazao ya baharini, Nd. Juma Khamis Jafar, amewataka wafanyabiashara hao kufuata taratibu za kisheria kwa kukata leseni na hati miliki kwa wakati, ili kuepusha usumbufu katika harakati zao za kila siku.

Kwa sasa hifadhi ya Pweza ipo Mkoa wa Kusini katika Vijiji vya Kisiwapanza na Kuukuu Kangani, na inategemewa hivi karibuni kuanzishwa katika kijiji chaFundo katika Mkoa wa Kaskazini na utasimamiwa na Jumuiya ya Mwambao na kuwa endelevuhadi kumalizika  kwa maeneo ya Kisiwa cha Pemba.

Comments