Wajasirimali wadogo wadgo Kisiwani Pemba wameiomba Serekali
kuendelea kuwapatia elimu ili kuweza kukuza mitaji yao.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizri mapema leo
hii wajasiriamali hao wamesema kuwa kupatiwa nafasi za kushiriki katika mafunzo
mbali mbali kunawezesha kujenga uzoefu wa biashara wanazozifanya nakuweza
kujikwamua hali ngumu za kimaisha.
Time Hamada Saidi mkaazi wa Shumba ya Mjini Wilaya ya Micheweni
amesema kuwa ameweza kufanya shughuli
zake za ujasiriamali kupitia mafunzo ambayo ameyapata kutoka katika taasisi
mbali mbali za kiraiya na kiserekali.
Amefashamisha kuwa kupitia mradi wa GAWE umemuwezesha
kujua kutunza kumbukumbu jambo ambalo awali hakuweza kufikiria kabisa juu ya utunzaji huo.
Nae Fatma Khamis Ameir Mkaazi wa Wete amesema ipo haja
kwa wajasiria mali ambao wemepata mafunzo kuweza kuyatumikia vyema kwa lengo la
kuimarisha biashara zao nakuondokana nadhana yakuwa mafunzo niyakujipatia fedha
pekee.
Aidha ametoa wito kwa wajasiriamali kutokuvunjika moyo nabadalayake kujiendeleza na kuondokana na hali ngumu ya kimaisha huku wakijua biashara nikitu gani jambo ambalo litamuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Skiliza hii=========>
Skiliza hii=========>
Comments