Mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecki Sadiki alisema hayo wakati wa Kikao cha
Ushauri cha Mkoa (RCC) ambacho kilikuwa maalumu kwa suala la hifadhi ya
mazingira.
“Kikosi cha usalama barabarani kiandae mpango wa ukaguzi wa
magari ya wanafunzi kila Jumamosi na yale yasiyo na sifa yaondolewe
barabarani....hatuwezi kukaa kimya huku tunaendelea kupoteza maisha ya
watoto wetu kama ilivyotokea mkoani Arusha” alisema.
Sadiki alisema Serikali ilisikitishwa na vifo vya watu wasio na hatia
kwani pia katika ajali hiyo mkoa wake uliguswa kwa kupoteza watoto 14.
Alimtaka Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issa kusimamia
kikamilifu ukaguzi huo ili kuepuka udanganyifu.
Ajali ya basi la shule Lucky Vicent ilitokea Mei 6, 2017 katika eneo
la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu mkoani Arusha na kusababisha vifo vya
wanafunzi 32 pamoja na walimu wawili na dereva wa basi hilo.
Jeshi la polisi mkoani Arusha tayari limeeleza chanzo cha ajali kuwa
pamoja na mwendo kasi, lakini pia wanafunzi na walimu hawakuwa wamefunga
mikanda jambo ambalo lingepunguza athari za ajali.
Aidha, Kamanda wa
Polisi wa mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema pia gari hilo
lililokuwa na uwezo wa kubeba watu 30, lilibeba 38 kinyume na uwezo wake.
chanzo:habarileo.
Comments