Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein afanya uteuzi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohammed Shein amemteua Bwana Shaaban Seif Mohamed kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Maafa ya Zanzibar.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Shaaban Seif Mohamed alikuwa Msaidizi Mrajis wa Bodi ya Hospitali Binafsi katika Wizara ya Afya.

Bwana Shaaban Seif Mohamed amechukua nafasi ya Bwana Ali Juma Hamad ambae atapangiwa kazi nyengine.


Uteuzi huo umeanza tarehe 20 Mei, 2017.
chanzo:zanzibar24.

Comments