
Kwa muijibu wa Ikulu, Rais Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli waliwatembelea wagonjwa hao saa moja asubuhi wakitokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako walihudhuria ibada ya Jumapili.
Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali ni Mzee Francis Kanyasu (Ngosha), mzee anayeaminika kubuni Nembo ya Taifa pamoja na mtoto Shukuru Kisonga ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa usiofahamika uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na maziwa.
Rais Magufuli alisema serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na changamoto zinazowakabili madaktari na wauguzi.
“Jamani, madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha, kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu,” alisema Rais Magufuli.
chanzo:zanzibar24.
Comments