
Ziara hiyo ya Dk. Shein inatarajiwa kuanza kesho tarehe 7 na kumaliza
tarehe 9 nchini humo ambapo ataanza ziara yake kwa kufanya mazungumzo
na mwenyeji wake Rais wa Djibout Ismail Omar Guelleh.
Aidha, katika ziara yake hiyo, Dk. Shein atatembelea miradi mbali
mbali ya maendeleo nchini humo ambapo miongoni mwa miradi hiyo
atakayoitembelea ni Bandari ya Doraleh, Bandari ya Ziwa Assal, Maeneo
Huru ya Uchumi pamoja na Kampuni ya Simu na Mawasiliano “Djibouti
Telecom Haramous”.
Katika ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali
akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Usafiri, Balozi Ali Abeid Karume, Waziri wa Afya
Mahamoud Thabit Kombo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afika Mashariki Dk. Susan Alphonce Kolimba.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi
Zanzibar (ZIPA) Salum Khamis Nassor, Mshauri wa Rais Masuala ya
Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia
Abdiwawa pamoja na watendaji wengine wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kurejea nchini Jumaatano Mei 10, 2017.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
chanzo: zanzibar24.
Comments