Ripoti iliyotolewa leo Jumanne na shirika la kutetea haki za binadamu
la Human Rights Watch imesema kuwa, raia hao waliuawa katika
makabiliano kati ya makundi hasimu ya waasi katika mkoa wa Ouaka,
katikati ya nchi.
Lewis Mudge, Mtafiti wa masuala ya Afrika wa shirika hilo amesema
watoto wanne wa familia moja akiwemo mtoto wa miezi saba ni miongoni mwa
raia waliouawa mwezi Machi na kundi la wapiganaji wa Fulani Union for
Peace in Central Africa.
Haya yanajiri siku chache baada ya Jeshi la Ulinzi la Uganda UPDF
kuanza kuondoa askari wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao
wamekuweko nchini humo tangu mwaka 2012.
Wanajeshi hao walikuwa miongoni mwa askari 3,000 wa Sudan Kusini na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, waliokuwa wakishirikiana na jeshi la
Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wamekuwa wakiwasaka waasi wa genge la
Kikristo la LRA akiwemo kiongozi wao Joseph Kony.
chanzo:parstoday.
Comments