
Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.
Kupaa
kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za
kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang.
Bw
Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango
waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.
Alikuwa
awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi.
Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya White House alisema baadaye
kwamba mazingira kama hayo, yanayoweza kufanikisha mkutano wa Trump na
Kim hayapo.
Korea Kaskazini imeongeza kasi katika majaribio yake
ya makombora na silaha za nyuklia miaka ya karibuni licha ya marufuku ya
Umoja wa Mataifa.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Han
Song-ryol aliambia BBC awali kwamba Korea Kaskazini inaamini kwamba
silaha zake za nyuklia zinaweza "kuilinda" dhidi ya tishio la shambulio
la kijeshi kutoka kwa Marekani.
Korea Kaskazini inahofia kwamba Marekani na Korea Kusini wanaweza kutumia nguvu kumuondoa madarakani Kim Jong-un.
Jumatatu,
Japan ilituma meli ya kubwa zaidi ya kivita baharini, hatua yake ya
kwanza ya aina hiyo tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata
iliyowezesha taifa hilo kuanza kupanua uwezo wa jeshi lake.

Meli hiyo ya Marekani
inaelekea kufikisha mafuta kwa meli nyingine za taifa hilo zinalohudumu
eneo hilo, ikiwemo meli yake kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson na
meli zinazoandamana na meli hiyo karibu na rasi ya Korea.
Korea Kaskazini imetishia kuizamisha Carl Vinson pamoja na nyambizi ya Marekani, huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka eneo hilo.
Aidha, taifa hilo lilifanya jaribio la kurusha kombora ambalo
lilifeli Jumapili, licha ya kuonywa mara kadha na Marekani na nchi
jingine dhidi ya kufanya majaribio ya makombora au majaribio ya silaha
za nyuklia.

Meli
ya kutekeleza mashambulio baharini ya Ufaransa iliwasili kusini
magharibi mwa Japan Jumamosi kwa mazoezi ambayo yatashirikisha majeshi
ya majini ya Japan, Marekani na Uingereza.
Comments