Ndani ya muda si mrefu kanuni za kuendesha mitandao (Blogu) zitakamilika.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wizara yake ipo mbiaoni  kukamilisha kanuni zitakazo simamia mitandao (Blogu) inayoendesha shughuli zake kama vyombo vya habari vya kieletroniki (Tv na Redio).

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali  na wanataaluma wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

“Hii media nyingine ambayo inafanya kazi zilezile kama za vyombo vya habari vya eletroniki, lakini nadhani tulikuwa hatujaamka kutunga kanuni, lakini nauhakika ndani ya muda si mrefu hilo litafanyika…lakini litakuwa zoezi shirikishi kama nilivyo ahidi…,” alisema Waziri Dk. Mwakyembe.
 chanzo:zanzibar24.

Comments