
Awali, Jeshi la polisi lilimtia mbaroni kijana Omar S. Omar mwenye
umri wa miaka 27 mkazi wa Bububu wilaya ya Magharibi A akiwa anasambaza
unga huo na ndipo alipomtaja Bi. Kei kama mmiliki wa unga huo, hata
hivyo mwanamke huyo alikimbia makazi yake hayo.
Kamadna wa polisi mkoa wa Mjini magharibi Hassan Nassir Ali amesema
“Mapambano haya yanayofanywa katika wilaya zetu za mjini magharibi dhidi
ya madawa ya kulevya, ni mapambano endelevu”
Aidha kamanda huyo ameiomba jamii kutoa mashirikiano kwa jeshi la
polisi ili kutokomeza vitendo hivi vinavyofanywa na baadhi ya watu.
chanzo:zanzibar24.
Comments